GET /api/v0.1/hansard/entries/895778/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 895778,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/895778/?format=api",
    "text_counter": 296,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "kazi, nyingi zao hazina wenye taluma yakuzitumia. Kwa hivyo, hawapati faida. Mashini hizi zimelala na serikali za kaunti zinalipa madeni lakini hazifanyi kazi. Rais katika Hotuba yake angeleta jinsi ya kutatua jambo hili lakini hakuleta. Hii imekuwa ni hasara tupu kwa serikali za kaunti. Sisi kama Maseneta tunazingatia umuhimu wa kuona ya kwamba serikali za kaunti zinafaidika na pesa ambazo tunapigania hapa. Ikiwa serikali za kaunti zitapata hizo pesa, ni makosa sana kwa Serikali Kuu kuzifuata ilhali mashini hazifanyi kazi na hazina faida yeyote katika hospitali za kaunti. Bw. Spika wa Muda, ningependa kuguzia hali mbovu iliyoko katika hopitali zetu. Tunajua mambo ya ugatuzi yalipelekwa katika serikali za mashinani. Lakini, vile vile, serikali Kuu lazima ijukumike. Kuna shirika moja linaitwa Kenya Medical SuppliesAuthority (KEMSA) ambalo lina siasa. Lina takiwa kupeleka madawa hospitalini lakini ukifika katika hospitali kuu ya Kilifi, utapata dawa kama vile Panadol au Septrin . Hakuna dawa zozote ambazo Serikal Kuu inapeleka katika hospitali za mashinani kupitia KEMSA. Kazi ya shirika hili ni kuchukua pesa tu. Magonjwa yaliyoPwani hivi sasa ni kama vile Malaria na Tuberculosi lakini, wanapeleka dawa kama vile pain killers ambazo haziwezi kusaidia yeyote. Bw. Spika wa Muda, Hotuba ya Rais ilikuwa sawa lakini ilikuwa na mtafaruku au mkosi fulani. Hakuweza kuhimiza shirika ambalo linapeleka madawa katika serikali za mashinani lipeleke dawa zinazofaa. Mwisho, ningependa kuguzia jambo muhimu kwa Wakenya. Rais aliguzia na kuelezea vizuri kwamba hatarudi nyuma kuhusu daraja la Wakenya kushikana mikono ili twende mbele. Tafakari hilo ni muhimu sana. Ningependa Mheshimiwa Rais alishike kwa mikono miwili kwa sababu hiyo wanayoita kushikamana mikono au Building"
}