GET /api/v0.1/hansard/entries/896255/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 896255,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/896255/?format=api",
"text_counter": 166,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ruiru, JP",
"speaker_title": "Hon. Simon King’ara",
"speaker": {
"id": 13468,
"legal_name": "Simon Nganga Kingara",
"slug": "simon-nganga-kingara-2"
},
"content": "hapa Bungeni. La muhimu ni kuwa kiongozi wa nchi alitambua ugatuzi kama njia mwafaka ya kuleta maendeleo katika maeneo mengi nchini. Tayari, Serikali kuu imepatia serikali za ugatuzi Kshs1.7 trilioni. Hii inamaanisha kuwa kuna shida kwa sababu asilimia 67.5 imetumika kwa mambo ya kawaida na si maendeleo. Ni vizuri serikali za ugatuzi ziangalie na kuona kiwango kikubwa kimetumika katika maendeleo na si mambo ya kawaida. Rais alizungumzia kuhusu mambo manne muhimu kama vile usalama, makaaji bora, viwanda na kilimo. Alisema kuwa huo ndio utakuwa mwelekeo wa kujimudu kama Wakenya wakati tunaongea juu ya maendeleo. Vile vile, aliongea kuhusu mambo ya afya. Alisema kuwa kumekuwa na majaribio katika kaunti za Kisumu, Garissa, Isiolo na Nyeri kuona vile wanaweza kujimudu kiafya. Jambo hili linafaa kutiliwa mkazo kwa sababu nchi hii haiwezi kuendelea kama sekta ya afya haijapewa kipaumbele. Eneo langu la Ruiru liko na kiwango kikubwa cha watu ambao wanakadiriwa kuwa laki sita na maeneo ambayo yametengwa kwa sababu ya afya ni manne pekee. Itabidi Serikali itilie uzito mambo ya afya katika maeneo yaliyo na watu wengi ili waweze kufanya kazi. Kazi haiwezi kufanywa ikiwa watu ni wanyonge. Hilo ni jambo ambalo sisi kama Wabunge lazima tulizingatie na kuhakikisha maeneo yaliyo na watu wengi yamehudumiwa kiafya ili kuwe na maendeleo."
}