GET /api/v0.1/hansard/entries/896258/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 896258,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/896258/?format=api",
    "text_counter": 169,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ruiru, JP",
    "speaker_title": "Hon. Simon King’ara",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": "Vile vile, Rais aliguzia mambo ya kilimo na akaongea juu ya kahawa. Alisema kitengo maalum kimebuniwa ili kiweze kusaidia wakulima wa kahawa kuendelea kushughulikia kahawa. Kwa maoni yangu, ni vizuri tuangalie mambo mengine yanayohusu kilimo. Kwa nini tunakubali mayai kutoka nje ilhali sisi wenyewe tunaweza kufuga kuku wa mayai? Ni vizuri sisi kama viongozi tutenge kiwango fulani cha fedha ili tusaidie wanachi wanaofuga kuku ili tuweze kukabiliana na watu wanaoleta chakula kutoka nje. Inawezekana kuwa nchi zinazotupatia chakula zimetenga fedha za kuwasaidia wakulima. Pia Rais aliguzia mambo ya masomo. Hakuna maendeleo yanayoweza kufanyika bila masomo. Katika eneo Bunge la Ruiru, masomo yako chini kwa sababu hakuna vifaa vya kutosha vya masomo. Kuna madarasa ambayo yana wanafunzi mia mbili. Waalimu watafundisha vipi? Inafaa kile kitengo katika Wizara ya Elimu kiangalie yale maeneo ambayo yametatizika zaidi ndiyo tuweze kujimudu kimaendeleo. Ninaunga mkono na ninafurahia vile Rais aliongea juu ya mambo ya uwiano; Wakenya wote kufanya mambo kama kikundi kimoja. Ninaunga mkono Hoja hii."
}