GET /api/v0.1/hansard/entries/896321/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 896321,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/896321/?format=api",
    "text_counter": 232,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Ahsante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ya kuzungumzia Hotuba ya Rais. Mwanzo, ningependa kumpongeza Rais. Alizungumza kama watu 100 hata zaidi ya 1,000. Alizungumza kama kiongozi. Alizungumzia mambo ambayo yatatuleta pamoja. Nchi nyingine Afrika zinatutaja vibaya kwa sababu ya mambo mawili ambayo Rais alizungumzia. Wenzetu wanatusengenya. Hapa Afrika Mashariki, wanasema shida yetu Wakenya ni kwamba baada ya uchaguzi, tunagombana kisha tunarudi nyuma. Ikiwa majirani wanatuona Rais akizungumza, kwa nini watu wasione amezungumza jambo zuri. Jambo la pili majirani wetu wanatuzungumzia vibaya ni ufisadi. Kupata uwiano na nchi nyingine inakuwa vigumu kwa sababu wanatuogopa. Ikiwa Rais ametambua na kuzungumzia hilo suala, tunafaa tumuunge mkono mia kwa mia. Rais amefanya kazi. Mimi na Mheshimiwa Mishi hatukuweza kuangaliana kwa macho kwa sababu ya mirengo ya kisiasa. Saa hii, tumefanya Harambee. Nilimwita Katibu wa COTU, Atwoli, akaja akanifanyia Harambee ambayo haijawahi kufanywa kwa miaka yote tangu tupate uhuru. Akina mama kule Lamu hawajafanyiwa Harambee kama hiyo. Vita ambavyo tumepata leo kutoka kwa Mheshimiwa Duale ni kwa sababu ameona kina mama wa Lamu wameinuliwa na kuwa sawasawa na kaunti nyingine. Hilo limeanza kuwakera. Kina mama wa Lamu wameinuliwa kwa kuwa wamepata pesa kima cha Kshs10,700,000. Hilo ndilo muhimu. Na hata wakija tena kufanya Harambee nyingine, tunawakaribisha. Waje tushindane kwa mazuri, pesa ziingie Lamu Kaunti nayo iwe sawasawa na kaunti nyingine. Ninataka kuwatahadharisha wale ambao watakuja Lamu wahakikishe kuwa wakija, wasishikane na walanguzi wa madawa ya kulevya. Tatizo kubwa tulilonalo kule Lamu ni ulanguzi wa madawa ya kulevya. Vita vinavyotokea kwa wingi Lamu ni kwa sababu ya madawa ya kulevya. Wanaouza wanajulikana. Katika eneo Bunge la Lamu East, watu ambao wanauza dawa za kulevya ni wawili. Mmoja ni Mr. Hamza Asman Ali. Anaharibu watoto wa watu wa Lamu na anajulikana. Serikali pia inamjua mpaka imempatia bunduki kumaliza watoto wetu. Kwa hivyo, ninamtahadharisha Mhe. Duale akija Lamu, asiunge mkono walanguzi wa dawa za kulevya. Watoto wetu wameisha Lamu na tunataka suluhisho. Ninaomba Serikali…"
}