GET /api/v0.1/hansard/entries/896555/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 896555,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/896555/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mwatate, ODM",
"speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": " Shukrani, Bw. Spika kwa kunipatia fursa hii. Mwanzo kabisa, kwa upana, Hotuba ya Rais ilikuwa ya kufana. Hata asilimia themanini kwa mia ninamuunga mkono. Ni maswala tu hapa na pale ambayo alikuwa ayashughulikie halafu angepata alama tisa kwa kumi. Mhe. Spika, wengi hapa wanalia kwa ukosefu wa chakula kwa sababu ni taabu kukipata. Lakini Mwenyezi Mungu alitupatia hewa na maji bure. Kule kwangu sehemu ya Mwatate kupata maji ni shida. Kuna matatizo makubwa tunapochimba visima kwa sababu ya ukosefu wa hela kwa vile kaunti yetu ni ndogo. Tunapata maji ya visima yakiwa na madini. Hata watu wengine wanatuambia kwamba tukinyua hayo maji, basi baada ya miaka kumi kwenda mbele, wakati visasi vyetu vitakuwa vinapata watoto, hao watoto watakuwa hawana mapua, midomo na kadhalika. Tumejaribu kila namna. Tunapoongea juu ya usawa wa nchi, inafaa Rais aangalie pembe zote za Kenya. Inafaa tuangalie wale ambao hawana maji ili wapewe ndio chakula ifuate na maswala mengine. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}