GET /api/v0.1/hansard/entries/896557/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 896557,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/896557/?format=api",
    "text_counter": 137,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mwatate, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "Kamati za Bunge ambazo zinahusika na maji na bajeti zinafaa kuwa makini sana. Kenya ni yetu sote. Ni lazima tuangalie ni wapi hakuna maji ili tuzibe hizo pengo ndio tuje kwa maswala mengine. Sasa hivi, ukiniambia juu ya barabara na sina maji, hiyo barabara itakuwa haina maana kwangu. Juzi hapa Bungeni wakati Rais aliongea kwa Kiingereza, kuna watu ambao walikuwa wanauliza kama tunaelewa. Katika hii Bunge, Wabunge zaidi ya asilimia 90 wanaongea Kiingereza na wale ambao wanaongea Kiswahili ni asimilia 10. Lakini ukienda kule nje, asilimia 90 ya wananchi wanaelewa Kiswahili na asilimia 10 ndio wanaelewa Kiingereza pekee."
}