GET /api/v0.1/hansard/entries/896559/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 896559,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/896559/?format=api",
    "text_counter": 139,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mwatate, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Andrew Mwadime",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "Lile swala la ufisadi alilisisitiza sana na sisi tunangojea tuone vitendo. Asubuhi nilimsikia mwenzangu akiongea kuhusu mihadarati. Hili si swala la kuchekesha, lakini ni swala mbaya katika pwani haswa Lamu. Hata kule kwetu sehemu ya Voi na kwingine, hili ni tatizo. Sasa hivi, Rais ameshikana na kinara wetu wa chama cha ODM na kwenda Uchina. Mtu kama mimi ninayetoka kabila ndogo siwezi kwenda Uchina, ilhali kule Voi, mpaka Taveta, reli inatakikana zaidi kwa sababu Arusha iko karibu ndiyo iende mpaka Rwanda. Je, nani atatusaidia watu wadogo kama sisi? Ninaomba pia ikiwezekana sisi Wakenya tubadilike. Juzi tumewapigia watu kura. Inafaa tuanze kufikiria kwamba ni bora Rais atoke kabila ndogo kama langu."
}