GET /api/v0.1/hansard/entries/896611/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 896611,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/896611/?format=api",
    "text_counter": 191,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie Hotuba ya Rais wa nchi ya Kenya. Ninamshukuru Rais kwa kazi nzuri ambayo amefanya katika nchi yetu. Pia, ninachukua nafasi hii kumshukuru Naibu wa Rais wa taifa letu la Kenya. Wenzangu wemeongea mambo kadhaa kuhusu utenda kazi wa Rais na matakwa ambayo ameweka mbele yetu tuone jinsi anapofanya kazi yake. Ninamshukuru kwa sababu ametambua Bunge letu kwa kusema kwamba Miswada 22 imetekelezwa katika Bunge. Ninamshukuru pia kwa kazi yake katika upande wa usalama. Mashinani wameweka mikakati ya kuwa na nyumba kumi kuhakikisha kwamba utekelezaji umefanyika katika sehemu tunakotoka. Lakini bado tuko na changamoto. Tuko na kamera ambazo zimewekwa katika maeneo kadhaa ya nchi yetu lakini hazisaidii maeneo mengine. Hivi majuzi, watu walienda katika benki moja hapa Nairobi wakaiba zaidi ya Ksh12 milioni. Bado tuko na changamoto kwa upande wa usalama nchini. Mwenzangu Mhe. Millie Odhiambo amesema kuwa watoto wetu, hasa wasichana, wananajisiwa. Jana kule Bungoma kulikuwa na kisa ambacho mama wa miaka 95 alinajisiwa. Hii ni baadhi ya changamoto kwa usalama wetu nchini. Wengine wamesema kwamba Katibu Mkuu hafanyi kazi yake lakini hayuko hapa kujitetea. Vile vile, Naibu wa Rais mwenye wanasema anahusika na mambo kadhaa, pia hayuko Bungeni kujitetea."
}