GET /api/v0.1/hansard/entries/896613/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 896613,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/896613/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Sisi kama viongozi tumepewa nyadhifa na wapiga kura tuje Bungeni na tunafaa kuwa katika msitari wa mbele kuleta amani na kuhakikisha tuna amani. Rais anataka tuende wote kama viongozi wa nchi hii bila kutenganisha wengine kwa manufaa ya ubinafsi. Pia, ningependa kuguzia elimu katika nchi yetu. Ninashukuru kwa sababu washikadau wanaosimamia elimu nchini wamekuwa katika msitari wa mbele. Sisi kama viongozi tunawaunga mkono ili watoto wetu wapate elimu ya kutosha na wale ambao wametoka katika shule za msingi waingia katika shule za upili. Tunafaa kuhakikisha wamepata haki yao ndio wakitoka hapo waende chuo kikuu na wapate haki zao. Hayo ndio matakwa yetu. Ninamuunga Rais mkono kwa hayo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}