GET /api/v0.1/hansard/entries/896726/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 896726,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/896726/?format=api",
"text_counter": 306,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, ufisadi unatumalizia wananchi wetu, na kutuletea balaa hapa nchini. Sio wote kule mashinani wanaweza kwenda kwa hospitali ambazo ni za kibinafsi. Watu wengi huenda hospitali za umma ili kuweza kuwezeshwa. Hata Mhe. Rais aliposema anazungumzia ajenda zake nne, moja ni kuhusu habari za kuwawezesha Wakenya kupata huduma ya afya kwa njia inayofaa na mwafaka."
}