GET /api/v0.1/hansard/entries/896855/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 896855,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/896855/?format=api",
    "text_counter": 116,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "kwa sababu tumeona amani na upendo katika taifa letu. Pia, tumeona sekta nyingi zikistawi. Vile vile, Rais alizungumzia mambo ya ugatuzi na akasema hatarudi nyuma. Ni jukumu letu kama viongozi haswa Bunge la Seneti, liwe chonjo kujua pesa ambazo zimetolewa katika ugatuzi zitamfaidi Mkenya. Kama Wakenya, tuweze kufanya kile tunaita kwa Kiingereza, socialaudit, ili tuweze kujua faida ambayo tunapata katika mambo ya ugatuzi. Vile vile, ningependa kuzungumzia wajibu wa kitaifa katika mambo yakiulimwengu. Kwa Kiiingereza, tunasema international obligations . Ninajua taifa letu limeweza kuweka sahihi mikataba tofauti tofauti, ikiwemo ule mkataba wa African Free Trade Area Agreements ambayo itatuwezesha kupata bidhaa na huduma kwa njia rahisi ikiwa tariffs zitawekwa chini. Vile vile, kuna mikakati ambayo ni itifaki ya East African Community ambayo kama taifa tumeshirikiana na ndugu zetu katika jumuiya ya East African Community . Ninataka niseme kama taifa, wakati tunaweka mikataba hii, ikiwa ni ya mataifa mawili ama zaidi ya mataifa mawili, lazima tuwe waangalifu. Ninasema hivyo kwa sababu ninaangalia mkataba wa madaktari wa Cuba na madaktari wa taifa letu la Kenya. Madaktari wetu waliweza kupata shida na changamoto sana. Nimeathirika kwa sababu nilipoteza kakangu ambaye alikuwa katika msururo wa madaktari kama wale. Tulipata changa moto sana wakati wa kifo chake kwa sababu walipokua wanamfanyia postmortem … Kwanza, sisi kama Waislamu hatufanyi postmortem . Hatukuulizwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}