GET /api/v0.1/hansard/entries/896862/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 896862,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/896862/?format=api",
"text_counter": 123,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "na kutakuwa na viwanda tofauti tofauti kama vile vya nguo za EPZ na viwanda vya ngozi. Viwanda kama hivyo vitaleta ajira nyingi kwa watoto wetu, haswa kwa vijana wetu. Mheshimiwa Rais alisema kutakuwa na Mswada unaoitwa Sovereign Wealth Funds Bill ambao utazungumzia yale mapato kutoka rasilmali zetu kama mafuta, gasi na madini. Tuna madini mengi sana kule Kwale na mafuta kule Turkana. Cha msingi, lazima tuangalie wakaazi na wenyeji wataweza kufaidika vipi na madini na rasilmali zile kupitia Mswada huu ambao utaletwa. Katika jambo la usalama, ninataka turejeshe zile programmes za NYS ili tuweze kuwapatia vijana wengi ajira. Vijana wengi wameingia katika magenge ya kigaidi."
}