GET /api/v0.1/hansard/entries/897210/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 897210,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/897210/?format=api",
"text_counter": 118,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa ugavi wa pesa za Serikali kwa muhula wa mwaka wa 2019/2020. Kwanza, ninaunga mkono lakini kwa masharti. Ni lazima ufanyiwe marekebisho kwa sababu mapendekezo ya Kamati ya Fedha ya Seneti yalipuuzwa wakati Mswada ulipopitishwa katika Bunge la Kitaifa. Mapendekezo kwamba pesa ziongezwe kutoka Kshs314 billion zilizotolewa mwaka huu mpaka Kshs335 billion. Mapendekezo hayo yalipuuzwa na Bunge la Kitaifa. Kupuuzwa huko ilikuwa ni dharau kwa Bunge la Seneti kwa sababu Seneti ndiyo inayoangalia maslahi ya kaunti zote. Bunge la Seneti ikisema kwamba pesa zinazotosha ni Kshs335 billion ni kwamba wamepima na wakajua kwamba ni sawa lazima ziongezwe. Ni lazima Mswada huu ufanyiwe marekebisho kuambatana na mapendekezo ya Bunge hili la Seneti. Jambo la pili ni kwamba tumeona kaunti zetu zimeweza kutoa huduma zaidi kwa wananchi katika Jamhuri ya Kenya. Hata hivyo, huduma hizo haijaambatanishwa na ugavi wa pesa zinazokuja katika kaunti hizi. Hatuwezi kusema kwamba huduma zimeboreshwa katika kaunti wakati pesa zinazotolewa zinazidi kupungua. Bw. Naibu Spika, tukiangalia kila sehemu katika kila kaunti, ijapokuwa ufisadi pia unaongezeka, tunaona kwamba huduma zinapatikana katika kaunti hizi. Huduma hizi zinahitaji pesa na kila aina ya msaada kutoka kwa Serikali kuu pamoja na wafadhili wa kutoka nchi za nje. Hatuwezi kupunguza pesa zinazokuja katika kaunti zetu kwa sababu huduma pia zinapungua. Jambo la tatu ni kwamba katika hizi kaunti zetu zote tumeona pia kwamba hili suala la vifaa vya afya imekuwa ikitumika vibaya na Serikali kuu kwa sababu vifaa vile vinaletwa bila ushauri mzuri kutokana na kaunti zile. Kwa hivyo, zile pesa zilizotengwa kwa huu mradi wa vifaa vya afya zitolewe na ziongezwe katika ule ugavi ambao utatolewa kwa Serikali za kaunti."
}