GET /api/v0.1/hansard/entries/901101/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 901101,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/901101/?format=api",
"text_counter": 140,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kitutu Chache South, FORD – K",
"speaker_title": "Hon. Richard Onyonka",
"speaker": {
"id": 128,
"legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
"slug": "richard-onyonka"
},
"content": "Pesa za NG-CDF zimeleta maendeleo Kenya. Kwa wale ndugu zangu wako hapa Wabunge, mimi nimechaguliwa kutoka eneo wakilishi la Kitutu Chache Kusini kwa sababu kazi ambayo hela zetu za NG-CDF zinafanya zinawaridhisha wananchi kunipigia kura mara tatu mfululizo. Nitawapa heshima sana wazee walioanzisha kazi hii kama Mzee Jimmy Angwenyi na wale Wabunge wengine ambao walishika doria na kuuliza Rais Kibaki kuhakikisha kuwa hizi hela ambazo zimeenda mashinani zilianza kufanya hivyo miaka kumi liyopita. Hela hizo zimefanya kazi. Vile ndugu yangu, Mheshimiwa Mbadi amesema, ingekuwa vizuri kwanza kama tungeongezewa hela hizi za NG-CDF. Asilimia 2.5 haitoshi. Kazi ambayo inafanyika wakati huu ni kazi ya kujenga mashule. Serikali imeleta nia na njia ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wote ambao wamemaliza darasa la nane wanaenda kidato cha kwanza. Inaonekana kuwa lazima tuanze kujenga mashule mengi na kuhakikisha wanafunzi hao wanaenda shule vilivyo. Kwa kumalizia, Wabunge walio hapa, tafadhali mhakikishe kuwa mwaka ujao tuongeze hela za NG-CDF zifike asilimia tano ili hizi pesa ziendelee kusaidia wananchi wa kawaida. Vile Mhe. Mbadi amesema, huwa hatuoni ni kitu gani serikali za kaunti zinafanya na mabilioni ya pesa zinazopata. Ukiangalia pesa ambazo Mbunge anapewa, hazizidi Kshs75 milioni, lakini zinafanya kazi nzuri na wananchi wanaridhika. Namshukuru Mhe. Mawathe ambaye nilimfanyia kampeni kule Embakasi. Kitu ambacho kilinishtua kule Embakasi ni hiki: Wakati Mawathe alikuwa Mbunge kabla ya kura zake kuja, aliendeleza vitongoji duni kule Embakasi Kusini. Ukiangalia ile kazi ambayo ilifanywa hata mimi nilishtuka. Kwa hivyo ningependa kumsihi ndugu Mawathe aendelee kuwasaidia wananchi wake. Ukiangalia yale majina ameyatoa hapa ambayo yatapitishwa na hili Bunge ni wananchi kutoka makabila mbali mbali hapa Kenya. Inaonyesha kuwa ndugu Mawathe kama Mbunge wa Embakasi Kusini si mkabila ila ni Mkenya halisi."
}