GET /api/v0.1/hansard/entries/901962/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 901962,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/901962/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Ndugu yangu, Mhe. Duale anasema kuwa hafahamu lugha yangu, lakini ningeomba zile dakika zilizobaki niweze kutoa duku duku langu, nisije nikazungumza kwa lugha ambayo pengine ni ya hasira nikaambiwa ni saumu. Ni zile hisia za hawa watu wanaojaribu kutuchukua sisi. Ukienda katika maeneo, anapotoka Mhe. Duale, ni mfano wa kuuziwa mifugo kwa kuonyeshwa wayo wa wale mifugo waliopita. Unaambiwa kwa kuangalia mfugo ule amepita hapa, amewanda na ukiangalia zile kato vile alivyoweza kupita pale… Kule kwetu mfano mwingine unaoweza kutumiwa ni kupelekwa katika bahari kisha uone yale mawimbi yanavyopigwa, mvuvi aanze kukuuzia samaki akuambie hapa kuna sulisuli, kolele, papa na nyangumi nitakuuzia kwa kuangalia tu jinsi yale mawimbi yanavyopiga. Ni muhimu sana Kiongozi wa Walio Wengi…"
}