GET /api/v0.1/hansard/entries/901967/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 901967,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/901967/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": " Ningependa tu kueleza kuwa lau wangekua na nia safi, Mswada huu ungeletwa kwa njia yaa kisawasawa sio kwa njia ya Mswada kumba. Huu Mswada Kumba ukiletwa, njia na madhumuni na nia ilikuwa ni Mswada kama huu ukiwekwa huwa ni Mkusanyiko wa sheria tofauti tofauti lau kuna mabadiliko ya herufi na mambo madogo madogo ambayo hayana uzito wa maana hivyo. Lakini leo kupeleka Mswada kama huu kwa kupitia njia hii, ni njia ya ulaghai ambayo inatumika. Watarejea hapa. Ningependa kulielezea Bunge kupitia kwako wewe Spika kuwa huu Mswada ukibadilishwa, njia na madhumuni ni nini? Serikali ya Japan ilitoa bilioni 27 kukajengwa terminal mpya kule Mombasa na kukaandikwa mkataba. Katika ule mkataba, walielewana kuwa lau kutakuwa na nia ya kuwa shirika ambalo si KPA kuendesha terminal ile basi kulikuwa kutumike Public, Private Participation, ile Act iweze kutumika. Leo tunajaribu kuletewa mashirika ambayo niya kibinafsi kutumia njia ambayo si sawa. Lugha watakayotumia ni kuwa njia hii ni kuweza kuleta Kenya National Shipping Line. Mbele yangu, kuna stakabadhi ambazo zimeletwa katika kamati tofauti za Bunge; kuna karatasi zenye kuonyesha hii Kenya National Shipping line ni ya nani. Asilimia 74.3 inafaa kuwa ya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}