GET /api/v0.1/hansard/entries/901977/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 901977,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/901977/?format=api",
"text_counter": 217,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": " Unajua tatizo hapa ni kuwa kila mmoja hujifanya kuwa Spika katika Bunge hili. Ningeomba tu niweze kutaja jambo lingine hapa kwa sababu katika hisia ambazo wanajaribu kutumia, hawa mabwana; la kwanza na la pili wanasema kutakuwa na nafasi za kazi. Suala lile tunajiuliza sisi, hatukatai na hakuna anayepinga ya kuwa ni sawa tuwe na maendeleo na kuwe na usawa katika nchi. Kwa nini iwe ni kampuni moja pekee yake ambayo imepatiwa nafasi hii bila ya kuwa na mkataba wa maana ambao umefuata sheria? Kwa nini ikiwa tunataka kupeana port yetu kwa kampuni kwa sababu KPA imeshindwa kuiendesha, kwa nini kusiwe na competitive bidding? Natumia lugha hii ili kuwakumbusha na kuwafahamisha Wakenya. Kwa nini kusiulizwe na kuwekwe makaratasi ya kuambiwa ya kuwa kampuni ambayo inataka kufanya kazi hii lazima ihakikishe imeajiri watu elfu kumi kazi. Jambo la pili tunataka kujua ni, mtatoa fedha ngapi kutupatia? Ukitaka kujua ulaghai, katika Bunge hili hili, kupitia sahihi yako, niliuliza swali hapa na ukapeleka suala hili kwa wenye kuhusika, ya kuwa kuna mashirika ya nje badili ya kuajiri Wakenya wanaajiri watu ambao sio Wakenya licha ya kuwa Wakenya wana uwezo wa kufanya kazi zile. Majibu tuliyoyapata na niko tayari kwa sababu haya majibu yana muhuri wa Bunge. Majibu ambayo yaliletwa na Waziri husika na aliyekuwa msimamizi wa Kenya Maritime Authority ni kuwa wanakubali kuna tatizo na wakaelezea ya kuwa wako katika hali ya kubadilisha sheria."
}