GET /api/v0.1/hansard/entries/902107/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 902107,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/902107/?format=api",
"text_counter": 347,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": " Sawa, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kulingana na uwezo wako na kulingana na hali ya Kiswahili, nitazungumza Kiswahili adhimu na sitaunganisha lugha nyingine yeyote. Maana ya “in totality” ni kwa jumla. Kwa hivyo nimejirekebisha na kusema “kwa jumla”. Neno “James” ni katika lugha ya Kizungu sijui niseme Jemsi Nyikal. Ni yale ambayo Mhe. Nyikal, na vile vile Mhe. Millie Odhiambo, walipinga. Katika Mswada huu kuna mambo ambayo yananigusa binafsi. Kama Mbunge kutoka kule Mombasa, tumempa uwezo mkubwa sana huyu Waziri katika mambo ya bandari. Hali hii itatuumiza sisi kama wakazi wa Mombasa, ambako bandari ipo. Hivi sasa, mdahalo mkubwa unaoendelea ni kuhusu Kenya National Shipping Line (KNSL) kuungananishwa na Mediterranean Shipping Company (MSC). Jambo hili si la sawasawa kwa sababu hakuna usawa. Katika bandari ya Mombasa hivi sasa, kampuni ya Maersk Line, ambayo yatoka Uholanzi, inabeba shehena asilimia 40 ya shehena za Serikali. Vile vile, Pacific International Line (PIL) inabeba takriban asilimia 15. Nashangaa ni kwa nini KNSL isisawazishwe na zile kampuni nyingine. Ni kwa nini MSC inafanya kazi yote? Naona hata ndugu yangu, Mbunge wa Mvita, Abdullswamad, anapiga makofi kunipongeza kwa sababu ni jambo la sawa. Ijapokuwa ni mimi ninayezungumza, yeye ana fikra hizo hizo: kwamba, ni lazima kuwe na usawa wa mambo haya. Kabla ya kuingia katika siasa, nilifanya kazi katika bandari. Ni lazima tuangalie kwa umakini kwa sababu pesa zote ambazo zinaingia kwa MSC zinakwenda katika nchi yao ya Italy. Pesa nyingi ambazo zinaingia katika Maersk Line zinakwenda Uholanzi. Pesa zinazoingia katika kampuni za meli ambazo zimefungua ofisi hapa nyumbani zinapeleka pesa zile katika nchi zao tofauti tofauti. Kenya National Shipping Line iliundwa mwaka 1989. Madhumuni yake ilikuwa kuangalia jinsi tutakavyokuwa na laini yetu ambayo itabeba shehena zetu. Kwa hivi sasa, kama alivyosema Mhe. Millie Odhiambo, kuna watu watapeli ambao wanataka kuingia pale na kuona jinsi watakavyopata commission na mambo ya tenda. Mediteranian Shipping Company, Maersk Line, PIL na kampuni kama Global Container Line zipo. Wanafanya kazi kutoka nchi zao na kuja katika bandari yetu ya Mombasa. Nashangaa mpaka sasa hakuna mabaharia ama vijana wetu wowote ambao wameandikwa katika hizo"
}