GET /api/v0.1/hansard/entries/902795/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 902795,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/902795/?format=api",
"text_counter": 240,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kulikuwa na umuhimu wa kuwepo kwa The Warehouse Receipt System Bill. Tukipitisha Ripoti hii itakuwa imepitia bunge zote mawili. Sisi kama Wabunge tuna kiapo kimoja kwamba tutakuwa waaminifu kwa Jamhuri ya Kenya na Katiba yake. Sioni kwa nini kuwe na mvutano baina ya Mabunge haya mawili. Wenzetu walipokutana kule Mombasa, walitumia fursa hiyo kutukashifu. Walisema kwamba sisi hatufanyi kazi yetu kama Senate. Katiba imetoa mwongozo kwamba kuwe na bunge mbili; Seneti na Bunge la Taifa. Tunajua kila Bunge lina kazi yake. Katiba pia inasema kuwa iwapo Mswada utapitishwa katika Bunge moja na ukataliwe katika Bunge jingine, tunafaa kuwa na Kamati ya Uwiano ili kuchunguza mahali kuna shida na mapendekezo yao yanafaa kukubaliwa na bunge zote mbili. Kwa hivyo, mwongozo wa Sen. Ndwiga unafaa kufuatwa na kamati zote za Senate."
}