GET /api/v0.1/hansard/entries/902799/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 902799,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/902799/?format=api",
"text_counter": 244,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "wa Wengi katika Seneti alipeleka kilio matangani. Hiyo ni sawa na kupeleka kilio matangani kwa sababu yeye kama Kiongozi wa Wengi katika Seneti anakaa katika the Senate Business Committee (SBC). Kwa hivyo, wao ndio viongozi wa Seneti. Wamechukua hatua gani kuhakikisha kwamba malamiko yetu yanafikia ofisi husika? Wangeandika barua ya malalamiko kwa Mkuu wa Sheria, Spika wa Bunge la Taifa na Ofisi ya Rais kwamba Sheria hiyo ilipitishwa bila ya kujadiliwa na Seneti kama inavyoeleza Katiba. Kwa hivyo kuja hapa kutulilia haitasaidia chochote kwa sababu tayari sheria imepitishwa na sisi kama Bunge la Seneti inafaa kuwapa mamlaka ya kusonga mbele ama aidha kuandika barua ya malalamiko kwa Mkuu wa Sheria kwa kuruhusu sheria ile kuwekwa sahihi na Rais bila kufuata Katiba. Kazi yetu kubwa ni kulinda masilahi ya kaunti. Haya ndiyo masilahi ya watu wengi ambao tunawawakilisha katika Bunge hili la Seneti. Ni lazima tulinde masilahi yao. Lazima katika hizi taasisi mbili; Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa, kuwe na heshima katika ofisi ambazo tunaendesha kwa sababu sisi sote tumeapa kiapo kimoja, tunaongozwa na Katiba na tunachukua mwongozo kutokana na Katiba hiyo. Kwa hivyo, ni lazima kuwe na heshima ile tunaita kwa Kiingereza “mutual respect.” Heshima hii itafanya kila mtu akitekeleza majukumu yake kulingana na Katiba."
}