GET /api/v0.1/hansard/entries/902802/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 902802,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/902802/?format=api",
"text_counter": 247,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Ugatuzi ni kitu kizuri kabisa ambacho Wakenya wote wanaliunga mkono sana. Wakenya wameukumbatia kwa moyo wote. Wakati huu, kama kuna mtu yeyote ambaye anataka kuharibu ugatuzi, basi atakuwa ameguza nyoyo za watu wa Kenya. Ugatuzi mahali ulipofikia wakati huu, ni ugatuzi safi ambayo ukitoka juu, unakanyaga chini na wale ambao watakuwa na nia ya kuongeza mambo mengine kwa ugatuzi, watakuwa wanaweka uzito mkubwa kwa watu wa Kenya."
}