GET /api/v0.1/hansard/entries/902974/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 902974,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/902974/?format=api",
"text_counter": 19,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "na National Housing Corporation (NHC) hususan National Housing Estate Magongo, wakaazi wamekuwa wakipata shida sana. Kodi zimeongezwa ilhali wanaishi katika hali duni. Nyumba zao zimeezekwa au zimefunikwa juu na mabati ya asbestos ambayo inadhuru afya ya binadamu. Bw. Spika, huu ni wakati mwafaka wa kuunga mkono maombi ya watu wa Kisumu kwa sababu maswala ya nyumba yanaathiri sehemu zote za nchi. Ujenzi was nyumba ni mojawapo ya Big Four Agenda ya Serikali. Lakini utapata mpaka sasa nyumba ambazo watu wengi wanaishi hususan wafanyikazi wa Serikali ni duni sana. Kwa mfano, nyumba zote katika Mbaraki Police Line zinafaa kupigwa marufuku kwa binadamu kuishi. Polisi wanaishi katika nyumba zilizo katika hali duni kuliko zile ambazo watu wanaishi katika maeneo ya vitongoji duni. Ni lazima Serikali itoe mwongozo kuhusiana na maswala ya nyumba. Kama Serikali ingetaka kuwapa wananchi makaazi, ingeanza na wafanyikazi wa Serikali, ili kila mmoja wao aishi nyumba ambayo mwanadamu anastahili kuishi."
}