GET /api/v0.1/hansard/entries/903090/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 903090,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/903090/?format=api",
    "text_counter": 135,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa ya Sen. Cherargei wa Kaunti ya Nandi. Kwanza ninalaani kitendo cha polisi chakumkamata Seneta wa Kakamega pamoja na aliyekuwa waziri wa michezo na Mbunge wa Matungu, kufuatia ghasia zinazotokea katika maneo ya Matungu. Kama wabunge na viongozi, tuna haki ya kuheshimiwa na kupewa fursa ya kujiwasilisha katika Makao Makuu ya polisi ama mahali popote polisi atatuhitaji kuliko kutushika hadharani, kututia pingu na kutupeleka kama ambao ni wahalifu. Kisa cha Mhe. Gikaria, Mbunge wa Nakuru Mjini ni cha kusikitisha sana. Hii ni mara ya pili mwaka huu yeye kushikwa. Kila anaposhikwa, polisi wanamchukua kama mhalifu wa kawaida. Ninampongeza Mhe. Malalah kwa uzoefu wake wamazingira aliyokuwa nayo kwa muda mchache."
}