GET /api/v0.1/hansard/entries/904080/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 904080,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/904080/?format=api",
    "text_counter": 133,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "mahakama hazifai kutekelezwa siku za Jumapili, Jumamosi ama siku kuu rasmi ya Serikali. Tulitarajia kwamba hili donda sugu litatatuliwa na National Land Commission (NLC). Lakini Tume hiyo ilitumia muda wake wa miaka sita na ambao uliisha bila kuondoa tatizo kubwa la dhuluma za kihistoria kuhusiana na ardhi katika miji ya Mombasa na Kaunti za Kilifi na Kwale. Bw. Spika wa Muda, tungeomba Kamati ya Seneti ambayo itapatiwa jukumu la kuchunguza swala hili, iingilie kwa undani swala hili; ichunguze sehemu ya Kilifi na Pwani nzima ambako kuna dhuluma za kihistoria. Mpaka sasa miaka karibu kumi baada ya kuwa na Katiba mpya, dhuluma hizo hazijashughulikiwa. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}