GET /api/v0.1/hansard/entries/904081/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 904081,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/904081/?format=api",
"text_counter": 134,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Ningependa kuchangia Taarifa hii ambayo imeombwa na Mhe. Madzayo. Hili ni jambo la kusikitisha sana kwa sababu kwa sasa shida kubwa ambayo tuko nayo ni swala la ardhi. Utakuta mtu anaondolewa katika ardhi na nyumba yake kubomolewa siku ya Ijumaa au Jumamosi asubuhi. Hiki kitendo kilitokea huko Mtwapa na watu walionyeshwa katika runinga wakipigwa. Mwakilishi wa eneo la Mtwapa katika Bunge la Kaunti (MCA) ameshikwa na kutiwa ndani. Mimi niliona jambo hili likiwa mbaya sana. Swala hili lazima litatuliwe kwa haraka sana. Kamati itakayopewa jukumu la kuchunguza jambo hili inafaa kwenda huko Mtwapa kwenye hiyo ardhi, ijue chanzo cha hiyo shida ni nini. Utapata mtu anakuja na Cheti cha Kumiliki Ardhi na hata hajui hilo shamba liko wapi, kwa sababu ametoka mbali sana. Akikuja anawapa polisi “kitu kidogo” na watu wanavunjiwa nyumba zao."
}