GET /api/v0.1/hansard/entries/904142/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 904142,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/904142/?format=api",
    "text_counter": 195,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda. Ninataka pia kuezeka juu ya yale waliyoyasema ndugu zangu, Sen. Kang‟ata, Sen. Sakaja na vile vile Sen. Mutula Kilonzo Jnr. Kitu cha kwanza ni kwamba heshima sio utumwa. Tunawaheshimu sana magavana lakini ikifika wakati wanaanza matusi, inakuwa personal. Walimtukana marehemu mama wa Seneta. Hatutakubali jambo hilo. Hilo litakuwa limepita mpaka. Kwa hivyo, Bunge la Seneti lichukue hatua mwafaka ili tujue njia tutakayotumia ili hawa watu wafuate sheria zinazotakikana kikamilifu."
}