GET /api/v0.1/hansard/entries/904418/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 904418,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/904418/?format=api",
    "text_counter": 157,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii pia nichangie Mswada huu. Kwanza, ninamshukuru sana dada yetu, Seneta Pareno, kwa kuleta Mswada huu wa marekebisho ambao hatimaye ukiwa sheria utasaidia vitengo vingi sana katika Kamati ya Uwiano na Utangamano. Kwanza, tunazingatia amani. Tunakumbuka baada ya uchaguzi, nchi yetu ya Kenya ilikumbwa na taharuki za aina nyingi ambapo tulipoteza maisha ya watu wetu. Hakukuwa na amani na biashara nyingi za watu zilizoroteka. Hali ya kutojua kesho itakuwa namna gani ilikuwa imetanda kote nchini. Hivi sasa, naona mambo mwafaka ambayo dada ameyaleta hapa na marekebisho mengi ili kuona taasisi yetu hii itakuwa na sheria mwafaka zitakazoweza kutuongoza katika mambo ya uwiano na utangamano na watu wazidi kuishi kwa amani. Ni muhimu kukumbuka nyakati kama hizo tukiangalia katika sheria hii ambayo imewekwa hapa, katika ukurusa wa 683. Mswada huu unaweza kuzingatia zaidi mporomoko wa maneno ambayo yanaweza kuleta chuki na makabila kukosana. Mswada huu utatulinda haswa tukizingatia ya kwamba kumekuwa na mwelekeo mwema ulioanzishwa na Rais Uhuru Kenyatta na ‗baba‘ Raila Amollo Odinga walipopeana pambaja na kusalimiana vizuri. Tumeona ya kwamba, hivi sasa, tuko na ndugu Maseneta ambao wanaenda kila mahali katika nchi na kuwahimiza watu wetu kukaa kwa amani na ushirikiano ili nchi ipate kuwa na mwelekeo na maendeleo. Yote haya yakijiri, yatasaidia katika ugawaji wa mambo kama vile kazi. Hatutalalia upande mmoja ya kwamba kabila fulani limepewa nafasi na makabila mengine yamekosa. Hivi sasa, kama ni chakula katika nchi yetu ya Kenya, Rais anaweze kuchukua wakati wake kuona ya kwamba kila makabila yote 43 yameweza kupata ugavi huu wa keki ili kila mtu katika jamii aweze kujihisi kuwa yeye kuwa yeye ni Mkenya. Bw. Naibu Spika, tumeona ya kwamba matusi au matamshi ambayo yanaweza kuleta chuki na fitina za kikabila yanaweza kutukosesha sisi miundo msingi ya kuishi kama Wakenya tunaopendana. Hapo awali, nimetangulia kusema kwamba tumekuwa na hali ya sitofahamu. Hatukuweza kuona ya kwamba sisi kama Wakenya, ni lazima tuwe na sheria ambayo itaweza kutuleta karibu na kulinda masilahi ya kila Mkenya. Kwa hivyo, nikimalizia, Mswada ambao tunautazama ni umuhimu sana kwa mambo ya uwiano. Kisheria utaleta Wakenya pamoja na kukosoa utengamano. Katika Bunge la Seneti, sisi tunaunga mkono Mswada huu. Iwapo utapita, utaleta maendeleo ambayo tunatarajia, kama vile kuona Wakenya wakiishi kama jamii moja."
}