GET /api/v0.1/hansard/entries/904665/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 904665,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/904665/?format=api",
"text_counter": 197,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia arifa ya Sen. Pareno. Bw. Naibu Spika, hili swala la kulipwa ridhaa kwa wale wanoathirika na miradi ya Serikali limekuwa donda sugu sasa. Kule Mombasa, walijenga SGR ambayo imeweze kufanya kazi kwa muda wa miaka mbili. Lakini, mpaka sasa, kuna watu ambao hawajalipwa ridhaa ya ardhi yao. Pia mali yao ilichukuliwa wakati wa ujenzi wa reli lakini hawajahi kulipwa ridhaa. Hivi sasa, kuna mradi wa Magongo Road ambao unaendelea. Contractor tayari yuko kwenye mradi huo na amelipwa lakini wale ambao wameathirika hawajalipwa. Zile fidia ambazo zinatakikana kulipwa, zimetengenezwa kwa njia ambayo si sawa. Wengine wanalipwa pesa nyingi kwa nyumba ndogo na wenye ardhi na nyumba kubwa wanalipwa malipo ya chini. Mwaka uliopita, nilileta arifa na Kamati ya Ardhi ikamuita aliyekuwa Mwenyeketi wa NLC pamoja na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Reli la Kenya. Wote walilaumiana mbele ya Kamati. Watu walisema hawajalipa na kuleta majina na hali kadhalika. Swala hili limekuwa donda sugu. Miradi mingi ya Serikali inapangwa bila kuzingatia pesa ambazo zitalipa ridhaa ambao wataathirika na miradi kama ule. Kwa hivyo, ipo haja, ya Waziri wa Ardhi, kuja yeye binafsi kujieleza ni kwa nini watu hawalipwi haraka iwezekanavyo wakati ardhi zao zinapochukuliwa kwa sababu tumeona sasa hakuna makamishena wa NLC. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}