GET /api/v0.1/hansard/entries/90474/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 90474,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/90474/?format=api",
    "text_counter": 108,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Bett",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 157,
        "legal_name": "Franklin Kipng'etich Bett",
        "slug": "franklin-bett"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, ninafikiri ni maswali wala si swali. Ningetaka kurudia kwamba tunafahamu kwamba barabara hiyo imeharibika na ni tatizo kwa wasafiri kutoka Rumuruti-Maralal. Nimesema kwamba tumetenga kiasi cha Kshs30 milioni, na awamu ya kwanza imeenda kwa mwanakandarasi kwa jumla ya Kshs14 million na wanaendelea kukarabati sehemu ya Naibor. Huyo ndiye mwanakandarasi ambaye Mheshimiwa amesema kwamba anamwaga maram. Nitatuma maofisa wa Wizara kuangalia vile anavyofanya lakini lazima mtu alete maram aweke kwa barabara kabla ya kutandaza. Hakuna njia nyingine. Hiyo murram inahesabiwa ili ijulikane kwamba mwenye kandarasi anafanya vile inavyotakikana yaani anaweka maram ambayo ni kiasi kilichotiwa sahihi katika kandarasi. Mimi nitachukua jukumu la kwenda kuangalia barabara hiyo. Lakini ningependa kumjulisha Mheshimiwa kwamba nimeenda huko mara mbili kuangalia hiyo barabara na daraja ambazo zimeharibika na ninashughulikia jambo hilo."
}