GET /api/v0.1/hansard/entries/90478/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 90478,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/90478/?format=api",
    "text_counter": 112,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Bett",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 157,
        "legal_name": "Franklin Kipng'etich Bett",
        "slug": "franklin-bett"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, hilo ni swali nzuri. Tumekuwa tunawaza kama tunaweza kushirikisha, si Wizara ya Maji pekee bali Wizara ya Mazingira na Madini, Wizara ya Ardhi na Wizara ya Kilimo ili tushirikiane na kupambana na mafuriko ya mvua kwa sababu yanaharibu barabara sana. Kwa hivyo, hilo ni swali nzuri na ninalitilia maanani. Ninasema hivyo kwa sababu ukiangalia Barabara ya Narok-Mai-Mahiu inahusu Wizara hizo zote. Wakati ilipotengenezwa hawakuzingatia milima na wakati maji yalikuja yalibomoa barabara kama bado inajengwa. Kwa hivyo, tuko na hilo wazo na tutalifuatilia ili tusaidiane."
}