GET /api/v0.1/hansard/entries/90487/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 90487,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/90487/?format=api",
    "text_counter": 121,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ms. Leshomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Asante, Bwana Naibu Spika. Nashukuru Waziri kwa kukubali kwamba barabara hiyo iko katika hali mbaya. Waziri amesema kwamba wataweka barabara hiyo mchanga mpaka Naibor. Kwa nini Wizara haiwezi kutengeneza barabara hii mpaka Maralal? Pia, ningeuliza Waziri atengeneze barabara hiyo wakati huu kwa sababu ni mbaya zaidi. Je,Waziri atachukua hatua gani ili kuhakikisha kuwa wananchi wanasafiri salama kwa sababu kuna majambazi wengi katika barabara hiyo? Watu wengi wameuawa katika barabara hiyo na wengine kuporwa mali zao. Pia, kuna wanyama pori katika barabara hiyo. Juzi, wanafunzi ambao walikuwa wanatoka hapa waliponea kifo. Wanafunzi hao walivamiwa na simba ambao walizuia basi lao. Kwa bahati nzuri, jirani ambaye ni mzungu aliwaokoa. Waziri atachukua hatua gani ili kuhakikisha kwamba watu wetu wanasafiri bila uwoga? Pia, Waziri amesema kwamba ameenda huko mara nyingi lakini ameenda kwa kutumia ndege. Hakuenda kwa gari. Ningeomba Waziri atembelee sehemu hiyo kwa kutumia gari ili ajionee jinsi watu wanavyoteseka kwa barabara kwa muda wa siku tatu au zaidi. Ningeomba aende tu na gari kwa sababu akienda kwa miguu hatafika. Tunaona uchungu sana kwa sababu hatuna pahali pa kupita. Ningependa pia kuomba Waziri aende sehemu hiyo ili ajione vile daraja zote zimeharibika katika eneo hilo. Daraja zingine zimesombwa na maji. Bwana Naibu Spika, ninakuomba ukubali nilete picha ya barabara hiyo ili muone vile wananchi wanakaa. Ni kama kwamba sisi tuko Uganda. Hatuko hapa Kenya."
}