GET /api/v0.1/hansard/entries/90490/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 90490,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/90490/?format=api",
"text_counter": 124,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Bett",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 157,
"legal_name": "Franklin Kipng'etich Bett",
"slug": "franklin-bett"
},
"content": "Bwana Naibu Spika, maswali yote ni swali moja. Hivyo ndivyo nimesikia mimi mwenyewe. Ningetaka kutoa hakikisho kwa Mheshimiwa Leshomo. Kama ni kwenda kwa mguu, awe tayari aende na miguu, twende pamoja; kama ni kwenda kwa piki piki awe tayari ili twende pamoja; kama ni kwenda kwa gari awe tayari twende pamoja. Niko tayari kwenda huko. Pili, barabara itakarabatiwa kutoka Rumuruti mpaka Maralal lakini tumeanzia Naibor wakati huu. Hiyo haimaanishi kwamba tutamalizia Naibor. Itaenda kutoka Maralal mpaka Rumuruti na itabidi tutumie pesa ambazo tumetenga mpaka mwisho wake. Ikiwa hazitatosha, itatubidi tutafute pesa zingine ili tumalize ukarabati huo vizuri. Ningetaka kuwapa pole watu wa Samburu kwa sababu ya shida ambazo wanakumbana nazo wakienda au wakitoka kwao. Nitajaribu kabisa kusaidiana na wao."
}