GET /api/v0.1/hansard/entries/906487/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 906487,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/906487/?format=api",
    "text_counter": 25,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Gona",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "Shukrani Bw. Spika kwa kunipa nafasi hii kuwakaribisha wasichana kutoka Kaunti ya Tharaka Nithi. Naamini kwamba watajifunza mengi hapa. Naamini kwamba kuna viongozi watakaotoka miongoni mwao. Nawasihi wawe mfano mzuri tukizingatia mara nyingi shule nyingi huchomwa wakati wa mitihani. Nawahimiza wanafunzi hawa wawe na nidhamu. Wasiwe watovu wa nidhamu kwani wakikosa nidhamu, wanawapa wazazi wasiwasi, hasa mama, kwa sababu ndiye mwenye kuhangaika zaidi kuhakikisha watoto wake wamesoma. Naomba wanafunzi watakapotoka hapa wajue kwamba kuna viongozi waume na wanawake. Viongozi wanawake sana sana hufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja. Mbali na kuwa Maseneta, kuna kazi mbali mbali ambazo sisi hufanya. Ukihesabu Maseneta waliopo katika jumba hili hivi sasa, utakuta kwamba, wanawake ndio wengi kuliko wanaume. Hivyo ni kumaanisha kwamba wanawake wanajitahidi zaidi. Wanawake huangalia kazi zao kwa uangalifu na kwa wakati. Mbali na kazi nyingi walizo nazo, wanawake huhakikisha kila kazi imefanywa kwa wakati wake. Naamini wanafunzi hawa wakitoka hapa, watakuwa wamejifunza mengi kutoka kwetu. Muwe watoto wazuri tutakuja kuwatembelea siku moja. Asante Sana."
}