GET /api/v0.1/hansard/entries/906488/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 906488,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/906488/?format=api",
"text_counter": 26,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Asante Sana, Bw. Spika. Nachukua fursa hii kuwakaribisha wasichana kutoka shule ya upili ya Wasichana ya Chifu Mbogori. Bunge ni jumba la malumbano. Hili ni jumba ambalo watu huleta miswada tofauti mradi kuwasaidia Wakenya katika tabaka mbalimbali. Kuna changamoto kubwa katika nchi hii kwa viongozi akina mama kuchaguliwa katika kaunti na maeneo bunge. Ningependa kuwahimiza wanafunzi hawa wasife moyo. Wawe na ari na motisha ya kwamba, pia wao wanaweza kuwa viongozi. Akina mama ni viongozi manyumbani kwetu. Hao kama wazazi wa siku zijazo, walee vijana watakaotilia maanani haki za akina mama. Hilo lisipotiliwa maanani, kizazi kijapo, hakitakuwa na ushawishi wa kuhakikisha kwamba akina mama wanawakilishwa katika Bunge la Taifa, Seneti na bunge za kaunti. Uwakilishi wa akina mama bado haujagonga ndipo. Wakati watakapopata uongozi, wasiwe tu na ari ya kujilimbikizia mali, sifa na umaarufu, bali wawe na ajenda ya kuhakikisha kwamba wataleta mabadiliko katika jamii. Asante sana."
}