GET /api/v0.1/hansard/entries/906610/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 906610,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/906610/?format=api",
"text_counter": 148,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante sana Bi. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kuchangia katika taarifa hii kuhusu mfumo wa elimu iliyoletwa na ndugu yetu Sen. Khaniri. Wahenga walisema; ndovu wawili wakipigana, nyasi ndio huumia. Kwa ukosefu wa Prof. Magoha kukaa na ndugu hon. Sosion, kujadiliana na kupata msimamo wa kuwa elimu katika nchi hii ni muhimu zaidi kwa watoto wetu katika shule za msingi, ni jambo la kusikitisha. Prof. Magoha anaelewa kwamba katiba ya Kenya inasema kwamba ikiwa kuna mjadala wa aina yeyote, ni lazima watu wakae, waelezane, waelewane ili wapate njia ya kuenda mbele. Wazungu wanaita consultation . Jambo la kusikitisha ni kwamba, walimu wana chama chao cha Kenya National Union of Teachers (KNUT) na wana haki ya kusikizwa na Waziri wa Elimu. Imekuaje hivi sasa Waziri anaonyesha madharau kwa chama cha walimu ambacho kina haki ya kujadili na kuuliza jambo wanapoliona halifai. Prof. Magoha anawakosea sana Wakenya kwa kupuuza chama cha walimu. Bi. Spika, jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba, Prof. Magoha angekuwa anatueleza anatandaza nini kusaidia elimu ya Kenya. Kuna shule ambazo hazina madawati, karo za shule ziko juu na kuna watoto walemavu ambao hawawezi kuenda shuleni. Kuna aina nyingi sana za shida ambazo zinakumba watoto wadogo. Watoto wetu siku hizi wanalazimika kubeba mikoba kama mzigo za gunia kwa migongo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}