GET /api/v0.1/hansard/entries/906611/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 906611,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/906611/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bi. Spika, hata wewe ni profesa na ulienda shule lakini haukuwa unabeba vitabu vingi kama wanafunzi wa sasa. Wakati wetu, tulikuwa tunabeba vitabu kama sita au saba. Mwanafunzi alikuwa anafanya mtihani wa kitaifa katika masomo saba kisha anajiunga na shule ya pili kabla ajiunge na chuo kikuu. Bi. Spika, hivi sasa, watoto wetu wamepatwa na mzigo mkubwa. Wanalazimika kubeba magunia migongoni wakienda shuleni. Ni jukumu la Prof. Magoha kuona kwamba mzigo wa watoto wanaoenda shule umepunguzwa na sio kupigana na chama cha walimu."
}