GET /api/v0.1/hansard/entries/906648/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 906648,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/906648/?format=api",
    "text_counter": 186,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante Sana, Bi. Spika wa Muda. Ni jambo la kuvunja moyo sana jinsi Seneta mwenzetu alishambuliwa kiwango hicho, ilhali wale ambao walikamatwa kwa kuhusika na mashambulizi hayo waliachiliwa huru. Inaonekana kwamba Serikali haitilii mkazo mambo ya usalama; sio usalama wa Sen. Anuar pekee yake bali ni usalama wa Wakenya kwa jumla. Najua kwamba Sen. Anuar ni mwanachama wa Kamati ya Usalama ya Seneti. Kwa hivyo, ningependa kuiambia Kamati ya Usalama ichunguze hicho kisa ili waweze kujua kiini cha kitendo hiki ni nini. Ni kana kwamba Serikali haiangalii usalama wa mtu yeyote. Hi ni kwa sababu sio Sen. Anuar peke yake aliyeshambuliwa. Ukienda sehemu nyingi hata Laikipia, watu wamekuwa wakishambuliwa kiholela usiku na mchana. Watu wanauwawa na inaonekana ni kama Serikali imeshindwa kutekeleza jukumu lake la kuhakikisha usalama. Kazi ya Serikali yoyote duniani ni kuhakikisha kuwa kuna usalama wa wananchi na mali yao. Lakini sisi tunaishi kwa uoga. Huku Nairobi viongozi wanashambuliwa na ukienda mashinani pia watu wanashambuliwa. Sasa tunajiuliza Serikali inafanya kazi gani wakati jukumu lake kuu ni kuleta usalama. Tungependa Kamati ambayo itapewa hii shughuli ya usalama, iangalie kwa upana na marefu swala la usalama wa viongozi na kila mtu kwa sababu mtu yeyote akishambuliwa ni jukumu la serikali kujibu maswali. Asante sana, Bi. Spika wa Muda."
}