GET /api/v0.1/hansard/entries/908787/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 908787,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/908787/?format=api",
    "text_counter": 281,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi South, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Ken Chonga",
    "speaker": {
        "id": 13374,
        "legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
        "slug": "richard-ken-chonga-kiti"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Kwanza, ninataka kupeana kongole kwa Kamati ya Bajeti kwa kazi waliyoifanya nikijua kwamba si kazi rahisi. Ninaunga mkono Hoja hii kwa sababu kazi ya Bajeti ndiyo inayopeana mpangilio wa shughuli ambazo Serikali inatakikana kuendesha. Baada ya kupitia Ripoti hii, kuna swala moja ambalo ninaliona ni la muhimu na lazima nilizungumzie. Mhe. Naibu Spika, wewe na mimi tunajua umuhimu wa elimu. Wewe mwenyewe ni msomi. Uko na Masters Degrees zisizopungua tatu. Sasa unasomea degree nyingine. Hakuna taifa lolote ambalo linaweza kuendelea ikiwa halitawekeza kwa mpangilio wa elimu. Linalonisikitisha katika Ripoti ya mapendekezo ya bajeti ni kilio ambacho tunakipata kila mwaka. Ikifika wakati wa Bajeti, hela ambazo hutengewa kitengo cha elimu huwa hafifu. Nikizungumza hivyo, ninafahamu ni nini ambacho elimu inatufaidi nacho. Katika Ripoti hii, tunaona vile taasisi zetu za elimu kuu zimepewa hela ambazo hazitoshi, huku tukijua umuhimu wa elimu ni nini. Kule Kilifi County, ipo taasisi moja inayoitwa Ronald Ngala University. Ilizinduliwa mwaka wa 2003. Kufikia sasa, ni miaka kumi na sita na chuo hicho hakijamalizika. Haya yote yanajiri kwa sababu ya bajeti ambayo inapangiwa taasisi hiyo. Nikikumbuka, mwaka wa 2003, sikuwa hata ninajua kuwa siku moja ningekuwa Mbunge. Nimekuwa na matamanio kuona kwamba chuo kile kinatimia sio tu kuwanufaisha watu wa Kilifi pekee yao, bali watu wa Kenya nzima. Taasisi hiyo imejengwa kwenye ufuo wa bahari. Mbali na kuwa kituo cha mafunzo, taasisi hiyo pia itakuwa ni hoteli maarufu sana. Kuna majengo ambayo yanajengwa mbele ya hoteli ile ambayo yanafanana na hoteli zingine ambazo ziko duniani. Hayo majengo yatavutia sana watalii. Kama ambavyo unafahamu, Kenya imekuja na hii Hoja ya kuboresha uwekezaji ndani ya bahari. Ufuo wa Pwani ndio una bahari kubwa na tunatarajia kwamba utaleta wawekezaji na watalii wengi. Hivyo basi, tuko na jukumu la kuhakikisha kwamba vijana wanatayarishwa kwa kupata mafunzo mwafaka ambayo yataweza kuhakikisha wageni wanaotembea nchi hii wanapata mandhari mazuri na kuburudishwa na vitu ambavyo wangetaka kuviona. Hivyo basi, mbali na kwamba mimi ninaunga mkono Ripoti hii, lalamishi langu ni kwamba wakati tunapanga bajeti… Kamati ya kupanga bajeti, ningeisihi, haswa kwa upande wa elimu, iweke hela za kutosha. Ni aibu kubwa kwamba kila mwaka walimu wanagoma kwa sababu mishahara yao haitoshi. Aidha, pesa za kuendeleza shughuli za elimu hazitoshi. Hivyo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}