GET /api/v0.1/hansard/entries/911040/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 911040,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/911040/?format=api",
"text_counter": 661,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Hoja ambayo imeletwa mbele ya Bunge na Sen. Kibiru, Seneta wa Kaunti ya Kirinyaga, ambaye tulisoma naye Chuo Kikuu cha Nairobi. Hoja hii imekuja katika wakati mwafaka, kwa sababu kila mwaka kuna malimbikizi ya pesa na madeni katika kaunti. Serikali Kuu ya Kenya inazidi kuongeza madeni kwa sababu ya miradi ambayo inafanywa bila ya kukamilishwa. Bi. Spika wa Muda, kiasi cha Kshs360 billion sio pesa kidogo, ikikumbukwa kwamba Bajeti ya kwanza ya Serikali ya Mheshimiwa Rais mstaafu Kibaki ilikuwa Kshs240 billioni. Kwa hivyo, sasa tuna kiasi Kshs360 billioni ambazo hazikutumika. Hii ni kwa sababu wananchi hawajaweza kupata ile tunaita kwa Kingereza value for money kutoka kwa miradi hii ambayo haijakamilika. Tukiangalia miradi hii, ni kama ile iliyofanywa na Serikali za Wilaya zilizokuwa kabla ya kuingia katika serikali za ugatuzi katika mwaka wa 2012. Kuna miradi ambayo ilianzishwa na serikali za kaunti katika awamu ya kwanza, baina ya mwaka 2013 na 2017. Miradi hiyo imesimama kwa sababu wale magavana walioingia hawakuiendeleza."
}