GET /api/v0.1/hansard/entries/911043/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 911043,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/911043/?format=api",
    "text_counter": 664,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Ukitazama gazeti la jana la Daily Nation, utapata kurasa zaidi ya kesi kumi ambapo madalali wanauza mali ya Wakenya kwa sababu ya kushindwa kulipa mikopo. Mikopo yenyewe ni ya wale waliopewa kandarasi za kazi za kaunti au serikali na kushindwa kulipa hiyo mikopo, kwa sababu Serikali Kuu au serikali za kaunti zimekataa kuwalipa. Kutokamilishwa kwa miradi kwa wakati unaofaa kunaleta athari kwa serikali na uchumi wa nchi. Hii ni kwa sababu hatutatumia kikamilifu miradi iliyofanywa, ilhali pesa zimetumika na miradi kukwama. Kwa hivyo, Bi. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii kwa sababu itasaidia kuhakikisha kwamba serikali za kaunti na Serikali Kuu zinawajibika kuhakikisha kwamba miradi inayoanzishwa katika mwaka wa fedha wa serikali inakamilika kabla ya mwaka unaofuatia, ili wananchi wapate faida ya miradi ile. Pia, kuna miradi muhimu kama ya maji ambayo imekwama, na wananchi wanaendelea kukosa maji katika sehemu hizo."
}