GET /api/v0.1/hansard/entries/911044/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 911044,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/911044/?format=api",
    "text_counter": 665,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Juzi, Kamati ya CPAIC ilizuru Kaunti ya Samburu, ambako tulipata miradi mingi imekwama kwa sababu ya ukosefu wa fedha, ilhali kila mwaka tunaomba fedha za kuendesha miradi hii. Kila mwaka, watu wanatengeneza Annual Development Plans (ADP) ili kusaidia kutekeleza Vision 2030, ambayo ni ramani inayotumika na Serikali kuhakikisha tunapata maendeleo nchini. Kila miradi inapokwama, maendeleo yanabaki nyuma, na Serikali inashindwa kufikia Millennium Development Goals (MDGs), ambazo zimekwama katika Ruwaza ya 2030 katika mwongozo wa miradi ya Serikali. Ni muhimu kabla ya miradi mipya kuzinduliwa, ile iliyopangwa kufanyika katika mwaka fulani wa fedha za serikali ikamilishwe. La sivyo, ni muhimu kuweka hesabu ya kuhakikisha kuwa miradi hii imekamilika kabla kuanzishwa miradi mipya. Katika sehemu nyingi za kaunti, ile miradi iliyoanzishwa, kwa mfano na gavana aliyetangulia, haifanywi na gavana anayeendelea. Vile vile miradi ya NG-CDF iliyoanzishwa na Mheshimiwa aliyetangulia, yule anayeichukua anaigandamiza na hayuko tayari kuifanya miradi hiyo. Hii ni kwa sababu anahofia kwamba labda pesa nyingi zilitumika au aliyofanya miradi hiyo hakushauriana na watu."
}