GET /api/v0.1/hansard/entries/911045/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 911045,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/911045/?format=api",
    "text_counter": 666,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, Wabunge au magavana pia wanabagua sehemu ambazo hazikuwapigia kura. Utapata sehemu zilizopigia kiongozi fulani kura kwa wingi zinapelekewa miradi kwa wingi, na kule kwingine hakupati miradi yoyote. Kwa hivyo, jambo hili linasababisha kutokuwa na usawa wa maendeleo katika sehemu tofauti za kaunti moja. Kwa hivyo, hili ni donda sugu. Ni lazima tutafute njia mwafaka ya kuhakikisha kwamba miradi inakamilishwa kwanza kabla ya kuanzishwa miradi mipya na serikali za kaunti au Serikali Kuu. Vile vile, lazima maendeleo yasambazwe katika maeneo yote katika kaunti ama nchi kwa usawa, kwa sababu sote tunalipa kodi katika mfuko mmoja. Haiwezekani kwamba mfuko wenyewe ufaidishe sehemu fulani zaidi kuliko sehemu nyingine, wakati sote tumo katika Kenya moja. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}