GET /api/v0.1/hansard/entries/912948/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 912948,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/912948/?format=api",
    "text_counter": 308,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Mhe. Naibu Spika wa Muda, ni “Lamu East”, na si “Amu”. Kwanza, ningependa kumpongeza Mhe. Osoro kwa kuleta Hoja hii hapa Bungeni. Kwa kweli suala la barabara ni suala nyeti sana. Tunazungumzia uchumi nzima wa nchi. Kwa masikitiko makubwa, barabara zetu za Kenya… Kwanza, kabla hatujaingia katika suala la namna tutakavyo fundisha vijana wetu wakiwa shule, barabara zetu ni tofauti na za nchi zingine. Kwa hivyo, hata unapomfundisha mtu kuhusu barabara, zile barabara anazofundishwa na zile anaenda kukumbana nazo ni tofauti. Kitu muhimu ni Serikali kupitia wizara ihakikishe kwamba barabara zetu zimejengwa kulingana na mwelekeo na mwongozo unaotakikakana. Utapata mambo mengi ambayo yanahitajika kuwe na barabara. Udhaifu na makosa makubwa yanapatikana katika barabara zetu. Hii ndio sababu utapata ajali na matatizo mengi yanapatikana katika barabara zetu. Swala la vijana kufundishwa maswala ya usalama ya barabara wakiwa shuleni ni jambo la muhimu na linahitaji kuangaziwa pakubwa. Kama nilivyosema, barabara nikipengele muhimu katika uchumi wetu ambao unatumika hapa nchini. Unapotembea mahali popote katika nchi hii, lazima utatembea katika barabara zetu. Ni muhimu vijana hawa wakiwa shuleni wafunzwe ili waelewe jinsi barabara zetu zilivyo na vile wanavyotakikana kutembea katika barabara zetu wakiwa wachanga na hata watakapokuwa wakubwa. Leo watoto wadogo wakiwa katika shule za chekechea wanatumia barabara hizi kwenda shuleni. Utapata kwamba ikiwa vijana hawa hawatakuwa na elimu ama na ujuzi kamili kuhusu barabara hizi matatizo mengi yanachipuka. Itakuwa vyema vijana hawa wakiwa na ujuzi na uelewaji kuhusu barabara zetu. Jambo hili litasaidia pakubwa katika kupunguza maafa mengi ambayo yanatokea. Kwa hayo machache, ahsante."
}