GET /api/v0.1/hansard/entries/914230/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 914230,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/914230/?format=api",
    "text_counter": 543,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Ninawaomba wenzangu wanawake na pia Wabunge wa kiume tuungane kuhakikisha kuwa pendekezo hili lililoletwa hapa halitapita na tuache pesa hizi ziwe katika Tume ya Jinsia na Usawa ya Kenya. Masuala ya jinsia humu nchini na hususan ya wanawake, kila mtu anajua kuwa wamekuwa wakiumia kwa muda mrefu. Watoto wa kisichana wanaumia zaidi kuliko wavulana na ukiangalia takwimu, unaona kuwa jinsia hiyo inapata shida zaidi. Wasichana wengi zaidi hawaendi shuleni na kadhalika. Kwa hivyo, ninaomba tuunge mkono kuwa Tume hii isikatiwe pesa zake na pesa ziweze kubaki pale pale. Tupinge pendekezo hili."
}