GET /api/v0.1/hansard/entries/914250/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 914250,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/914250/?format=api",
    "text_counter": 563,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Tana River CWR, MCCP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13275,
        "legal_name": "Rehema Hassan",
        "slug": "rehema-hassan"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninaunga mkono watu wa IPOA wapatiwe pesa hizo lakini ninazungumza kwa masikitiko. Sioni kazi IPOA wanafanya kwa sababu mwaka jana, kuna vijana wa kwangu Madogo walidhulumiwa na sijaona wakichukua hatua yoyote. Watu watatu walikufa na kuna kijana wa miaka 20 ambaye amekatwa mkono kwa kupigwa risasi na askari wa polisi na mpaka saa hii, kijana huyo amezunguka akienda kwa IPOA Garissa. Mara anazungushwa akirudi, na mpaka saa hizi, hajapata haki yake. Kwa hivyo, kama watakuwa wanaongezwa pesa hizi ili wapate kula mishahara minono minono kwa nyumba zao na wananchi wanadhulumika, mimi hata sioni faida yake. Lakini ninaunga mkono wapatiwe pesa hizo wazidi kutudhulumu. Ahsante."
}