GET /api/v0.1/hansard/entries/915871/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 915871,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/915871/?format=api",
"text_counter": 343,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nataka kwanza kutoa shukrani kwa Kamati ya kusimamia masuala ya afya hapa Bungeni ambayo inasimamiwa na Mhe. Sabina Chege kama mwenyekiti kwa kuleta Ripoti hii ambayo ni ya muhimu sana. Tangu Kenya ipate Uhuru mwaka wa 1963, hadi kufikia mwaka wa 2010 wakati tulipata Katiba mpya, masuala ya afya yalipatiwa kipaombele kwenye Katiba yetu na ndani ya Katiba kulitajwa umuhimu wa kila Mkenya kuwa na haki ya kupata huduma ya afya kiwango cha kumwezesha kuishi vile anavyostahili. Ripoti hii ambayo imetengenezwa na Kamati ya Afya ni muhimu sana maana inagusia hospitali za kitaifa ambazo ziko hapa nchini. Tunafahamu kwamba hakuna hospitali kubwa kushinda Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta. Hakuna hospitali kubwa inayosimamia masuala ya ugonjwa wa akili kama vile hospitali ya Mathari. Vilevile, hakuna hospitali kubwa inayosimamia masuala ya ubongo na uti wa mgongo kama vile Hospitali ya Kitaifa ya kusimama masuala ya uti wa mgongo. Ukweli ni kwamba ukienda kwenye Bonde la Ufa, Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi pia inasimamia masuala ya matibabu kwa wananchi hapa nchini. Ukweli ni kwamba hospitali hizi hazipatiwi nafasi ya kufanya kazi zinazostahili kufanya. Kwa mfano, Wakenya wengi ni wale ambao wanapelekwa nje kwa matibabu kwa sababu hospitali hizi hazijapatiwa nguvu na kuwezeshwa kutibu Wakenya. Mimi sitaki kuongea sana maana wenzangu wameshaongea. Nataka kurejelea kwamba kuna umuhimu wa kuwa Bajeti zikitengenezwa, hospitali za kitaifa zipatiwe bajeti za kutosha. Vilevile, hospitali hizi pia ziwe na bodi ambazo zinataweza kuzisimamia na pia zipatiwe vyeti vya kumiliki ardhi maana mara nyingi wakitaka kujenga au kufanya lolote lile, wanashindwa. Hospitali ya Mathari ya kusimamia ubongo na hospitali ya kusimamia masuala ya uti wa mgongo zimeonewa sana maana hazina bodi ya kusimamia masuala yake. Vilevile, kufanya uamuzi inakuwa ni shida maana Wizara ndiyo inayofanya uamuzi kwa niaba yao, hivyo basi Wakenya hawawezi kupata huduma inayofaa. Wengi wamekwenda hospitali kama zile na wakitoka hapa wakienda nje wanatibiwa na wanapona. Lakini miaka nenda miaka rudi, wakiwa kwenye hospitali hizo hawawezi kupata matibabu. Ukifika katika Hospitali ya Mathari, utawahurumia wagonjwa na kuhuzunishwa na shida wanazopata na shida ambayo iko katika hospitali ya kusimamia masuala ya uti wa mgongo. Ripoti hii imetoa mapendekezo yanayofaa na serikali yetu ya Kenya ya Jubilee lazima ifuate mwelekeo huu. Wizara ya Afya na Wizara ya Ardhi lazima zitekeleze masuala yote yaliyotajwa hapa. Ninaomba kuunga mkono Ripoti hii. Asante sana."
}