GET /api/v0.1/hansard/entries/916662/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 916662,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/916662/?format=api",
    "text_counter": 222,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "hii. Ni jambo la kuhuzunisha muno kwa sababu ni kama tuko hapa kujadili tabia za “Jopo ama Kongamano la Kitaifa” ukifafanua the National Assembly . Parliament inamaanisha Bunge na sitaki kuongea kuhusu hilo. Ikiwa mapato ya nchi yanaongezeka, basi mgao wa pesa za kaunti unapaswa kuongezeka kwa asilimia hiyo. Kazi yetu kama Maseneta ni kutetea na kuhakikisha kaunti zetu zinapata pesa. Ningependa kuwaambia ndugu zetu walioteuliwa kwenye jopo la kushughulikia jinsi pesa zitatumiwa wasimame kidete ili kuhakikisha kaunti zinapata Kshs335 billion. Tusilegeze kamba kwa sababu tukifanya hivyo, tutakuwa tunaleta mfano usiofaa. Wao wameongeza pesa zao hadi Kshs100 million. Tukisema pesa za kaunti ziongezwe, wanaanza kutoa vijisababu ambavyo havina msingi. Tutatetea kaunti zetu kwa hali na mali na kwa damu na jasho. Hatutakubali mtu yeyote alete vijisababu na kupinga kuongezwa kwa pesa za kaunti kwa sababu ya ufisadi. Pia kuna ufisadi katika the National Government Constituencies Development Fund (NG-CDF). Hatujawahi kuwaambia kuwa wanatumia pesa vibaya na hawawezi kuongezewa kwa sababu kuna ufisadi. Kutokana na vijisababu hivyo, wana nia na mpango wa kupigana na ugatuzi. Mtu yeyote anayeguza ugatuzi anaguza Seneti na ukiguza Seneti unaguza Wakenya. Watu husema kuwa kabla ya mbwa kufa, hupatwa na kichaa. Akipata kichaa, hubweka na kuanza kula miti. Sitaki kusema mengi. Kuna watu katika nchi yetu wanaoonyesha mtindo wa mbwa anapotaka kufa kwa sababu wameshikwa na kichaa. Hiyo inamaanisha wanakaribia kufa."
}