GET /api/v0.1/hansard/entries/916743/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 916743,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/916743/?format=api",
    "text_counter": 303,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa fursa hii. Nimengoja sana kwa hamu. Kama Maseneta wenzangu walivyochangia, yangu ni kusisitiza tu tukae ngangari sisi sote. Kama ni kuenda kortini kama walivyosema Maseneta wenzangu, tuungane pamoja, tusimame imara na tuone Seneti imepewa heshima yake. Kama unavyojua, sisi Maseneta ndio jicho katika kaunti zetu humu nchini. Kuna watu fulani ambao wanaipinga hii Seneti. Hata hivyo, Waswahili walisema kwamba kila jambo lina mwanzo na mwisho wake. Ninawasihi Maseneta wenzangu tuungane, tuwe kitu kimoja. Tusimame tuhakikishe kwamba Seneti yetu inaheshimiwa. Si kila mara tunaambiwa hivi, kesho hivi, mara oversight na sisi wenyewe ndio tunafanya kazi kubwa sana katika kaunti zetu. Bw. Naibu Spika, sitaki kuchukua muda mwingi kwa sababu kuna wawili au watatu ambao lazima wachangie."
}