GET /api/v0.1/hansard/entries/917073/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 917073,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/917073/?format=api",
"text_counter": 253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Ningependa kuongea kwa Kiswahili kwa sababu ninaona Kimombo kimetembea sana na kuna wale watu wa mashinani wangependa kuelewa mambo ya Hoja hii. Kwanza kabisa, ninataka kuseme kwamba si tunataka kukejeli Bunge la Seneti ama tunataka kuleta sitofahamu katika Bunge la Seneti. Hii ni Hoja ambayo inataka kuweka mambo sawa, kulingana na Katiba yetu inavyosema. Katika Vifungu 95 na 96, Katiba yetu imezungumzia majukumu na nguvu za Bunge; kwanza, Bunge la Seneti na pili, Bunge la Taifa. Tumelileta jambo hili kwa sababu kumekuwa na dukuduku kwa wananchi kwamba “pengine pesa zetu zinatumika vibaya ama majukumu yanaweza kurudiana rudiana.” Kwa mtazamo wangu, nilifahamu kwamba Bunge la Seneti na lile la Kitaifa lingekuwa kama vile Uingereza ambapo kuna House of Commons na House of Lords . Nilielewa kwamba ile ilikuwa inaitwa House of Lords ni kama vile Seneti hapa kwetu Kenya – ni Wajumbe ambao, sana, wanapeana ushauri katika Taifa la Kenya, na Bunge la Taifa katika mambo ambayo yanahuzu nyanja tofauti tofauti. Kwa hivyo, lazima tujue majukumu ya Bunge la Seneti, haswa katika mambo ya Miswada ambayo inatusumbua sana. Tunaona Kifungu 110(1) kinazungumzia vizuri sana Miswada ambayo inahusika na Bunge la Seneti ambayo ni Miswada inayozungumzia majukumu na nguvu ambazo pengine zinaweza kuleta utata katika mambo ya kaunti. Pia, kifungu hicho kimezungumzia mambo ya uchaguzi wa Members of the County"
}