GET /api/v0.1/hansard/entries/917087/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 917087,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/917087/?format=api",
"text_counter": 267,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": " Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninataka niseme kwamba tukiangalia Ibara ya Nne, kwa wale hawatafahamu “Ibara” ni nini, ni ile “ FourthSchedule ”… Ibara hiyo imezungumzia haswa zile kazi ambazo zinahusu Bunge la Seneti kama kilimo, afya, usafiri katika kaunti na mambo mengi sana ambayo wenzangu waliotangulia wameyazungumzia. Vilevile, Ibara ya Nne imezungumzia yale majukumu ya kitaifa ambayo yanafanywa na Bunge la Taifa. Iwapo Katiba imezungumzia mambo haya kinagaubaga, kwa nini tuwe na sitofahamu? Kwa nini tuwe tunarudiarudia ama ile tunasema duplication wakati tunafanya kazi zetu kama Wabunge? Wakati mwingi sana, kuna suala limeangaziwa na Bunge la Seneti na Bunge la Taifa. Ripoti zinazokuja huwa tofauti na zinazoleta mg’ang’ano na tunakosa kupata mwelekeo. Ni wakati muafaka tujue sisi viongozi wa Taifa ambao tunajua majukumu yetu tujue kamati zile zitatengenezwa katika Seneti ziwe ni kulingana na majukumu, nguvu na kazi zao. Zile zitatengenezwa katika Bunge la Taifa, hili la National Assembly, iwe ni kulingana na majukumu na nguvu ambazo tumepewa na Katiba ya Kenya pasi na kwenda kinyume chake. Katika Kifungu cha 94, tunaona kwamba Bunge zote mbili zinahitajika kukubali na kulinda Katiba yetu. Katika Kifungu cha 3 cha Katiba, Mkenya anahitajika kukubali na kuilinda Katiba. Kuilinda Katiba ni kuilinda kwa kufanya zile kazi ambazo Katiba imetupa sisi kama Wabunge katika Bunge la Taifa na lile la Seneti. Katika Kifungu cha 110(3), Spika wetu na yule was Seneti, kila wakati, wanahitajika kuangalia suala la kujua Miswada ni ya kaunti au ni inayosimamia kupitia Bunge la Taifa. Kwa hivyo, sijui tunavurutania nini kwa haya mambo kila saa. Mambo ya kukagua walioteuliwa na Rais, tumeona ni jukumu la Bunge la Taifa linaloitwa National Assembly kulingana na Katiba. Kipengee cha 132(2) kinasema kwamba Rais atateua na sisi kama Bunge tutakagua iwapo aliyeteuliwa anaweza kufanya kazi ile. Lakini, tunaona hata Seneti wamekagua yule tunamuita Inspector General of Police (IG) juzi. Hapo tunaona tunaleta utata na sitofahamu katika mambo yetu kama watu moja. Je, sisi kama Wakenya tunaweza kuyapata mambo ya ugatuzi ambayo tuliweza kuwa na Seneti, ambalo jukumu lake kubwa ni kuangalia mambo ya kaunti 47? Kuna changamoto gani na tutaweza kuangalia nini? Kwa hivyo, mambo ambayo tunazungumzia, kwa mfano, kilimo, makavazi tunayoita Museums, leseni za pombe, wanyama na cemetery, tusiyaone kuwa ni mambo madogo. Haya ni mambo ambayo yanamdhuru mwananchi kila kuchao na anapata changamoto nyingi. Kwa hivyo, ni lazima tujue kamati tutakazotengeza, zitakuwa ni kamati kulingana na majukumu yetu ya kikatiba kwa mujibu wa vifungu 95 na 96 vya Katiba. Iwapo tutaenda kinyume na hayo, itakuwa si sawa. Wizara kama ile ya Defence ni wizara inayoangalia mambo ya kitaifa tu. Haiangalii mambo ya kaunti. Wizara ya Interior inaangalia mambo ya usalama wa kitaifa. Wizara ya"
}